NEWS AND ENTERTAINMENT

Search...

Followers

Feb 25, 2023

Tony Rashidi vuliwa mkanda wa ABU


 Rais wa  ABU, Houcine Houichi kupitia barua kwa umma amebatilisha ushindi wa Bondia Mtanzania Tony Rashid aliyetwaa taji la uzito wa ABU Super Batman na kumtangaza Solebo Ngebinyana wa Afrika Kusini kama mshindi.


“Jana usiku wa tarehe 24 Februari 2023 katika jiji la Dar es salaam Tanzania, taji la uzito wa ABU Super Bantam lilishindaniwa kati ya Tony Rashid (Tanzania) dhidi ya Sabelo Ngebinyana (Afrika Kusini).


“Kwa bahati mbaya, kutokana na makosa ya kimahesabu kwenye karatasi ya Mkusanyiko wa Kadi za Alama na Msimamizi wa pambano kama inavyoonyeshwa kwenye kiambatisho hapa chini, jina lilitolewa kwa mpiganaji asiye sahihi "Tony Rashid" (Tanzania) badala ya "Sabelo Ngebinyana" (Afrika Kusini).”


“Hivyo kwa taarifa hii tunasahihisha na kumtangaza SABELO NGEBINYANA (Afrika Kusini) kama mshindi wa pambano la hilo.” imesema taarifa hiyo.


No comments:

Post a Comment