NEWS AND ENTERTAINMENT

Search...

Followers

Jun 25, 2023

MWANAFUNZI ALIYEPOTEA MBEYA AKUTWA KWA BABA JOSE MUUZA MKAA.


Kutoka mkoani Mbeya Mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya Sekondori ya Panda hill, Ester Noah, amepatikana baada ya kupotea kwa siku zaidi ya 35. 


Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamini Kuzaga amesema Mwanafunzi huyo amepatikana majira ya saa tano asubuhi maeneo ya Ifisi katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbalizi akiwa nyumbani kwa Azurath Abdul Mfanyabiashara wa genge katika maeneo hayo.

ACP Kuzaga amesema Azurath ameeleza kwamba mtoto huyo alimpokea kutoka kwa kijana muuza mkaa ambaye amekua akimuuzia magunia ya mkaa akifahamika kwa jina moja la Baba Jose ambaye alimuomba aishi naye kwa siku mbili wakati akitafuta chumba ili aweze kuishi na mtoto huyo.

Akiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa, Juma Homera mwanafunzi huyo alipewa nafasi ya kujieleza ambapo aliwasihi walimu kuacha tabia za kunyanyasa wanafunzi.

#mohmedia72 


No comments:

Post a Comment